Povu linalotengenezwa na vyura
wadogo kwa ajili ya kulinda mayai yao linaweza kuponya majeraha ya
wagonjwa walioungua, wanasema wanasayansi.
Povu gumu linaweza
kukusanywa na kutumiwa katika mchakato wa matibabu kama kizuizi baina ya
bandeji na ngozi iliyoungua, wanaamini.
Watafiti katika Chuo kikuu cha Strathclyde wameanza majaribio ya sehemu ya povu hilo.
Wanafanya majaribio hao kwa kutumia povu kutoka kwa vyura hao wadogo kutoka kisiwa cha Tungara huko Trinidad.
Vyura hao kutoa povu la urefu wa sentimeta 5 kulinda mayai yao dhidi ya magonjwa na hali ya hewa kwa wastani wa siku tano.#
Povu hilo imetengenezwa kwa aina tano za Protini.
Doctor Paul Hoskissonna wenzake wanasema wameweza kuzichunguza aina nne za protini hizi na wameanza kuzichanganya na dawa zao.
Watafiti
hao watawasilisha kazi yao katika katika mkutano wa mwaka wa kituo cha
uratibu wa shughuli za utafiti wa viumbe hai -Microbiology Society
utakaofanyika Liverpool.
No comments:
Post a Comment