Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL
kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa
vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.
Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho
hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi
kuzifanya ili kuomba wayamalize.